Bwana Mpya Amponza Zari

YULE bwana mpya aliyemtambulisha kwa picha hivi karibuni mzazi mwenziye Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amemzulia msala wa aina yake mtandaoni.

 

Kilichotokea ni kwamba, mara baada ya Zari kuweka picha hiyo kwenye ukurasa wake Instagram, Wabongo wakaanza kumporomoshea matusi kwa kumwambia ameishiwa kiki atulie.

 

Mashabiki hao ambao wengi wanaaminika ni wa kutoka Tanzania, walimsema Zari kuwa amezidi kumposti jamaa huyo wakati yeye ni mtu mzima na mambo hayo angewaachia vijana.

 

“Mh! Mwenzetu naye amekuwa kama kina Rayvanny, haya mapichapicha angeachana nayo tu jamani.“Anafikiri kufanya hivi ni kumkomoa Diamond wakati Diamond mwenyewe hana mpango naye tena, anajisumbua tu,” aliandika shabiki mmoja ambaye anaonekana ni shabiki wa Diamond.

 

Mbali na huyo wapo baadhi ya mashabiki wachache ambao walionekana kumtetea Zari wakiwataka wale wanaomsema waache kwani kila mtu na uamuzi wake.Walisema kinachowatesa Wabongo wengi ni kutokupenda kuona Zari anafanya mambo yake mazuri na ukizingatia wao hawana.

 

“Wabongo umasikini unawasumbua tu, mtu bando lake, kaweka yeye mwenyewe sasa sijui wao kinawauma nini,” shabiki mmoja alimtetea Zari.

 

Licha ya mjadala kuwa mkubwa, Zari yeye hakutaka kuwajibu waliomponda zaidi ya kuwakomesha kwa kuposti picha nyingi za yeye akiwa na bwana wake huyo ambaye kimsingi bado hajamtambulisha jina.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

Toa comment