Bweni Lateketea, Wanafunzi Wanusurika

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Charlotte iliyopo katika Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro wamenusurika kuungua kwa moto baada ya bweni wanalolala wanafunzi wa kike wa kidato cha kwanza kuwaka na kuteketea kwa moto majira ya asubuhi wakati wakiwa madarasani.

Bweni la shule hiyo likiwa limeteketea pamoja na vifaa vyote vya wanafunzi. Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro SACF Goodluck Zelote amesema wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.


Toa comment