Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF limefuta mashindano ya fainali za Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17. Mashindano hayo yalitarajiwa kufanyika Morocco kuanzia Machi 13.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania cha vijana chini ya miaka 17 kilishawasili Morocco ambapo mchezo wa kwanza ulipangwa kuchezwa Machi 14 dhidi ya Nigeria.