The House of Favourite Newspapers

CAF Yaibana Simba Mechi ya El Merreikh

0

 

Klabu ya Simba SC itacheza bila mashabiki kwa mara ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan, ikiwa ni maelekezo kutoka shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambapo mchezo huo utachezwa Machi 16, 2021 katika dimba la Mkapa Dar es Salaam.

 

Michezo yote ya Simba waliocheza katika uwanja wa nyumbani msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wamecheza wakiwa na mashabiki kuanzia hatua ya awali mpaka kwenye mchezo mmoja wa hatua ya makundi, lakini mashabiki waliokuwa wanaruhusiwa ilikuwa ni asilimia 50 ya uwezo wa uwanja.

 

 

Kuelekea kwenye mchezo wa siku ya Jumanne, ambao ni mchezo wa pili Simba kucheza nyumbani katika hatua ya makundi, klabu hiyo imethibitisha kuwa mchezo huo hautakuwa na mashabiki yakiwa ni maagizo kutoka CAF.

 

 

“Wakati tunajiandaa na mechi hii tulipokea taarifa kupitia TFF, ambayo ilitoka shirikisho ala soka barani Afrika CAF, ikituagiza au ikituamuru mechi yetu ya tarehe 16 dhidi ya El Merreikh ichezwe bila washabiki,” amesema Haji Manara, Mkuu wa Idara ya Mawasiliana na Habari wa klabu hiyo.

 

 

Simba ndio vinara wa kundi hilo wakiwa na jumla ya alama 7, na mchezo uliopita walicheza dhidi ya wababe hao kutoka Sudan, mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu. Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni na utachezeshwa na waamuzi kutoka Afrika ya Kusini.

 

Leave A Reply