The House of Favourite Newspapers

Caf Yaruhusu Mashabiki 10,000 kwa Mkapa

0

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiruhusu timu ya Simba kuingiza washabiki 10,000 katika mechi yao ligi ya Mabingwa, dhidi ya AS Vita kutokana na maombi ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

 

Simba inatarajiwa kuikaribisha As Vita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia  Kongo (DRC) jumapili Aprili 3, kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa, Dar es Salaam.

Klabu ya Simba inaongoza msimamo wa kundi A wakiwa na alama 10, wakihitaji sare ili kujihakikishia nafasi ya Robo fainali, lakini wanahitaji kushinda mchezo huo ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya kuongoza kundi ili kuepuka adha ya kupangwa na vigogo kwenye hatua ya robo fainali.

 

Leave A Reply