Caf Yawapa Yanga SC Silaha Muhimu

SHIRIKISHO la Soka Afrika (Caf) wamewapa bonge la mchezaji Yanga baada ya kumruhusu kipa wao, Mkenya Farouk Shikalo kuanza kutumika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kumpiga ‘stop’ kutumika kwenye mechi za awali.

 

Shikalo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao walishuhudia dakika 180 za mechi zao dhidi ya Township Rollers ‘kideoni’ baada ya leseni yake kuchelewa kutoka. Wachezaji wengine ambao walikosa leseni ni pamoja na straika Mcongo David Molinga na Mustapha Suleiman.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa wamepata ruhusa ya kumtumia Shikalo ikiwa ni baada ya Caf kutoa leseni yake ambapo watamtumia kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Zesco United.

 

“Muda wowote kutoka sasa leseni ya Shikalo itawasili baada ya Caf kuruhusu atumike kwenye mechi inayokuja, lakini kwa Mustapha na Molinga wao bado na hatuwezi kuwatumia hadi tutakapofika makundi.

 

“Hakuna shaka kurejea kwa Shikalo baada ya kuruhusiwa kucheza anakuja kuongeza kitu kingine katika kikosi na kama unavyojua hii ni mechi ngumu. Timu kwa sasa ipo Mwanza na itakaa huko hadi siku tatu kabla ya mechi yetu na Zesco ambapo tumechagua kucheza nao Septemba 14,” alisema Ten.

Said Ally, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment