The House of Favourite Newspapers

CALISAH ATOA SIRI ATAKAVYOMLEA MWANAYE

Calisah Abdulhamiid

MWANAMITINDO Calisah Abdulhamiid ametoa siri jinsi atakavyomlea mwanaye, Calic kwamba atakuwa tofauti kabisa na watoto wa mastaa wengine Bongo ambao wanasifika sana mitandaoni.  Akizungumza na Mikito Nusunusu, mwanamitindo huyo alisema kuwa Calic akikua atakuja kuwa mtoto wa aina yake na wa kipekee ambaye itakuwa ngumu kumlinganisha maisha yake na watoto wengine wa mastaa.

“Mwanangu akikuwa kwanza sitegemei mtu yeyote kuja kumfananisha na hao wengine, kwa sababu nimejipanga kumlea kiutofauti kabisa kwa hiyo watu wasubiri tu wataona,” alisema Calisah.

Comments are closed.