CALISAH: MWANAMKE WANGU ANANITOSHELEZA

Calisah Abdulhamiid

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Calisah Abdulhamiid kwa mara ya kwanza amefunguka kwamba anampenda sana mpenzi wake Lisah, ambaye pia amefanikiwa kumzalia mtoto mmoja wa kiume aitwaye Calic na kwamba hategemei kabisa kuja kutengana naye kwa sababu ni mwanamke muelewa hata pindi anapokosa hela mfukoni.

Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto mwanamitindo huyo alisema kwamba, katika maisha ya kimapenzi kukoseana na kugombana kila wakati kupo, ila kikubwa kinachohitajika ni kusameheana na kuacha mambo yapite, hivyo mara nyingi anapogombana na mzazi mwenzake huyo hukaa chini na kumaliza tofauti zao.

“Mimi mwenyewe mara nyingi tu namkosea mpenzi wangu lakini mwisho wa siku tunaongea na kuyamaliza, pia mwanamke wangu sio mtu maarufu kabisa, hivyo huwa anapata shida sana anapokutana na skendo mbaya mitandaoni kuhusu mimi, lakini nashukuru Mungu ni muelewa huwa tunaongea na kuyamaliza, kwa hiyo sitegemei kuachana naye leo wala kesho kwa sababu pia amenizalia jembe la kuja kunisaidia baadaye,” alisema Calisah.


Loading...

Toa comment