Campus Night 2019: Alichokifanya MKHULULI wa SAUZI, Haijawahi Kutokea – Video

MUIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili raia wa Zimbabwe ambaye anaishi nchini Afrika Kusini, Mkhululi Bhebhe amefanya maajabu wakati akitumbuiza kwenye Kongamano la Victory Campus Night la mwaka 2019, ambalo limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers usiku wa leo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliofika kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kukutana na marafiki.
Mkhululi ambaye alishangiliwa na jukwaa zima wakati akipanda jukwaani kutumbuiza ameonyesha umahili mkubwa na kudhihirisha kuwa kweli ni mwimbaji wa Kimataifa baada ya kuangusha burudani ya aina yake jambo ambalo liliwaamsha mashabiki wake wote na kuanza kuimba nyimbo zake mwanzo hadi mwisho huku wakicheza na kushangilia kwa kusifu.
Licha ya mvua kunyesha, lakini mashabiki hawakuona kama ni shida, walivamia jukwaa na kuanza kucheza wakimsifu Mungu kwa matendo yake makuu.
Mkhululi alioyekuwa akisubiliwa kwa hamu na Watanzania kupanda jukwaani, aliimba nyimbo zake tatu kali ikiwemo Ichokwadi na Zvamaronga.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone limetikisa Jiji la Dar es Salaam licha ya mvua kunyesha lakini watu walijaa uwanjani na ratiba ikaenda kama ilivyokuwa imepangwa.

Katika tamasha hilo, ambalo limeanza majira ya saa 1:00 jioni, waimbaji mbalimbali wamepanda jukwaani kuimba wakimsifu Mungu baadhi yao ni, Upendo Nkone, Miriam Lukindo Mauki, Joel Lwaga, Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama, Ipyana Kibona na wengine wengi.
PICHA NA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

TAZAMA SHOO YA MKHULULI

Loading...

Toa comment