The House of Favourite Newspapers

Cannavaro akimbia, Kamusoko apewa kazi

0

kanavaro1MAMBO yamekucha sasa, kwani nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema wala hatahangaika kumzuia Hamis Kiiza wa Simba, badala yake kazi hiyo ataifanya, Mzimbabwe Thabani Kamusoko.

Cannavaro amewahi kucheza pamoja na Kiiza katika kikosi cha Yanga kabla ya straika huyo kutemwa Desemba, mwaka jana na sasa yupo Simba.

Tangu alipotua Simba, Kiiza ameonekana lulu ambapo hadi sasa amefunga mabao matano katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara. Leo Kiiza anaichezea Simba dhidi ya Yanga ikiwa ni mara yake ya kwanza kuivaa Yanga tangu alipoachwa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Cannavaro alisema binafsi anamuona Kiiza kuwa mchezaji wa kawaida kwani anamjua uzuri na ubovu wake awapo uwanjani, lakini kwa maelekezo kuhusu mchezo huu, Kamusoko ndiye atakuwa anamzuia straika huyo.

“Nimesikia taarifa za Kiiza za kutamba kuwa atatufunga, lakini ninachomwambia ni kwamba hatapata nafasi hiyo kutokana na mikakati tuliyoipanga kwa kuanzia kwa mabeki na viungo.

“Huyo nimemkabidhi Kamusoko atembee naye popote atakapokuwepo na mimi pamoja na Yondani (Kelvin) tumechukua majukumu mengine ya kumdhibiti mwingine atakayecheza na Kiiza, sisi hawezi kutusumbua kwani tunamjua vizuri tu,” alisema Cannavaro.

Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu mkakati huo wa Yanga, Kiiza alicheka kidogo kisha akajibu: “Hiyo hainiogopeshi, badala yake kama mshambuliaji nitatimiza wajibu wangu wa kufunga kwa kila nafasi nitakayoipata.”

Leave A Reply