The House of Favourite Newspapers

Cannavaro Amfuata Manji Mahakamani Kisutu -Video

0
Cannavaro akizungumza na Manji.
NAHODHA wa Klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, leo Septemba 18, ameibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kupata nafasi ya kuzungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji.
 

Cannavaro Amfuata Manji Mahakama ya Kisutu

 

Baada ya kutinga mahakamani hapo, Cannavaro alimuwahi Manji na kusalimiana naye kisha kupiga kuzungumza mambo machache ambayo hata hivyo haijajulikana kama walikuwa wakijadili mambo ya soka kuhusu klabu hiyo au la!
Wakipiga stori.
Klabu ya Yanga imekuwa ikiongozwa na Manji kwa miaka mingi ambapo baada ya kushtakiwa na kuwekwa rumande kwa miezi kadhaa kabla ya wiki iliyopita kuachiwa huru kwenye kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi ya Manji ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya Yapigwa Kalenda

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kubwa ya kuona Manji akiwa msitari wa mbele kuiongoza timu hiyo kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Manji alikuwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi yake anayotuhumiwa kujihusisha na matumizi madawa ya kulevya ambayo hata hivyo imeshindwa kusikilizwa na kusogezwa mbele hadi Septemba 25 mwaka huu.

MANJI Amshitua Okwi, Atia Neno Kuhusu Bosi Wake Huyo

Leave A Reply