The House of Favourite Newspapers

Cannavaro moto uleule Stars, Bocco arejea

0

JOHN BOCCONAHODHA wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia watashinda mechi dhidi ya Malawi na wasahau makosa aliyofanya katika mchezo wa kwanza.

Taifa Stars, kesho Jumapili itacheza dhidi ya Malawi mechi ya marudiano kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 ambapo ipo mbele kwa mabao 2-0 iliyoyapata katika mchezo wa kwanza.

Katika mchezo huo wa awali jijini Dar es Salaam, kuna wakati Cannavaro ambaye ni beki wa kati alionekana kufanya makosa kadhaa ambayo kama Malawi wangekuwa makini wangeweza kupata bao.

Akizungumza na Championi Jumamosi muda mfupi kabla ya kwenda Malawi, Cannavaro alisema: “Kweli kuna makosa yalifanyika katika mechi ya kwanza, kocha ameturekebisha na nakuhakikishia tutafanya vizuri.

“Mashabiki hawapaswi kuwa na hofu na sisi kwa yale makosa ya kwanza, tupo vizuri wakati huu.”

Wakati huohuo, straika John Bocco amerejea kikosini baada ya kupona majeraha ya kifundo cha mguu. Kutokana na majeraha hayo, Bocco aliukosa mchezo wa kwanza.

Leave A Reply