The House of Favourite Newspapers

#Carabao: Liverpool Yaifanyia Unyama Leicester

0

KLABU ya Liverpool imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la ligi baada ya kuiondosha Leicester City kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya 3-3.

Leicester City watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuumaliza mchezo huo kipindi cha kwanza walipokosa nafasi kadhaa za wazi licha ya kuondoka na uongozi wa 3-1 kabla ya Liverpool kubadilika kipindi cha pili na kusawazisha mabao hayo.

Sasa Liverpool watakutana na Arsenal katika nusu fainali ya michuano hiyo na mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Januari 4 au 5 mwaka 2022.

Leave A Reply