Cardi B Avunja Rekodi Tuzo za Grammy Miaka ya 2000
RAPA wa kike, Belcalis Marlenis Almánzar, maarufu kama Cardi B amevunja rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kike kupokea tuzo ya album bora ya rap kwa miaka ya elfu mbili, Februari 10 siku ya Jumapili katika ugawaji wa tuzo 61 za Grammy.
Katika kipengele hicho alikuwa anashindana na wasanii wakali katika game akiwemo, Pusha-T, Macmiller, Nipsey Hussle na Travis Scott .
Baada ya kupokea tuzo hiyo aliwashukuru wote waliohusika kutengeneza album yake kwa kuchangia hata mchango wa mawazo na washiriki ambao walikuwa kwenye kipengele kimoja kugombea naye tuzo.
Mwanadada Lauren Hill ndiye wa mwisho kunyakua tuzo ya kundi kwa album bora ya rap, ‘The Core’ mwaka 1995.
Baadhi ya marapa wa kike akiwemo Lil Kim na Remy Ma walitpa pongezi kupitia akaunti zao za tweeter.
Comments are closed.