Carlinhos Apewa Majukumu Mapya Yanga

SASA rasmi Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amembadilishia majukumu kiungo wake raia wa Angola, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’ kwa kumtoa katikati na kumpeleka pembeni.Awali, kabla ya kuja Kaze, kiungo huyo alikuwa akichezeshwa namba 10 na aliyekuwa Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic.

 

Mrundi huyo alianza kumtumia kucheza pembeni namba saba katika mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze alisema kuwa anafurahishwa na uwezo mkubwa alionao Carlinhos, lakini kwake atamtumia kucheza kama kiungo wa pembeni namba 7 au 11 baada ya kumuona hafiti namba 10.

 

Kaze alisema kuwa kiungo huyo ni mzuri zaidi akitokea pembeni akiamini nyota huyo atakuwa tegemeo katika kikosi chake katika kuelekea michezo ya ligi ya mzunguko wa pili kutokana na uwezo mkubwa wa kutengeneza mabao

akitokea katika majeraha.“Carlinhos alikuwa mzuri zaidi akitokea pembeni, bahati mbaya alipata majeraha na sasa anaendelea vizuri baada ya kupona majeraha yake na juzi alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports.

 

“Ni mchezaji mwenye mbinu sana, ni mzuri zaidi akitokea pembeni, naamini atafanya kile ambacho mashabiki wanakitarajia kutoka kwake na habari njema kwao ni kwamba amerejea kikosini.“

 

Ujio wa Fiston (Abdoul Razak) ndiyo utamuondoa katika nafasi hiyo kwani huyo ni mtu sahihi ambaye ataitendea haki namba 10, mwanzo nilijaribu kumtumia Carlinhos, Niyonzima (Haruna), Kaseke (Deus) na Farid (Mussa) wote walishindwa kuitendea haki nafasi hiyo,” alisema Kaze

STORI NA WILBERT MOLAND

Toa comment