The House of Favourite Newspapers

Carlinhos Arejea, Nabi Amuita Fasta

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amemuunganisha kwenye kikosi kitakachoenda Shinyanga, kiungo wake raia wa Angola, Carlos Carlinhos tayari kwa kupambana na Mwadui FC, kwenye mchezo wa kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho utaopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Jumanne ijayo, Yanga itashuka dimbani hapo baada ya kutoka kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya JKT Tanzania uliopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukiwa ni mchezo wa ligi kuu uliowafanya waifikie Simba iliyo kileleni, lakini wanazidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

 

Carlinhos aliumia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora dhidi ya Prisons ambapo alichanika msuli wa nyama za paja.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, Kocha Nabi amelazimika kumuunganisha kikosini Carlinhos baada ya kuridhishwa na afya yake ili aweze kuwa na uwezekano mkubwa wa kumtumia kwenye mechi zake zijazo.

 

Nilimsikia kocha akimwambia meneja ahakikishe Carlinh os anakuwa sehemu ya wachezaji watakaosafiri kwenda Shinyanga maana tayari ameonekana kuimarika jambo ambalo kocha amesema itakuwa vyema kama atajumuika nasi kwa ajili ya kujiweka sawa katika mechi zijazo,” kilisema chanzo hicho.

Musa Mateja,Dar es Salaam

Leave A Reply