The House of Favourite Newspapers

Carlinhos, Yacouba Wamoto Balaa Yanga

0

HABARI ziwafikie wale wote ambao w alidhani baada ya Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi kukabidhiwa kikosi hicho hatakuja kutabasamu baada ya kusimama Ligi Kuu Bara, safu ya ufungaji ikiwa butu, ambapo sasa mambo ni moto kwa Carlos Carlinhos pamoja na Yacouba Sogney.

 

Mwambusi yupo na wachezaji wake katika kijiji cha maraha, cha Avic Town Kigamboni ambako amejichimbia na wachezaji wake kwa ajili ya kujiandaa vilivyo na michezo ya Ligi Kuu Bara na ile ya Kombe la FA, iliyosalia baada ya kusimama ligi ikiwa kileleni na pointi zake 50.

 

Akizungunza na Championi Jumamosi Mwambusi, ameweka wazi kuwa, sasa mambo ni motoo kwa viungo washambuliaji wake, Yacoub na Carlinhos, ambapo tangu wameanza mazoezi wamekuwa wakionyesha hali ya kupanda kwa viwango vyao jambo linalompa matumaini ya kuja kufanya maajabu ligi ikianza.

 

“Tangu nimeingia kambini Jumatatu, baada ya kupumzika kwa takriban siku tatu ulipotokea msiba wa Hayati Rais Joseph Magufuli,

ashukuru sana wachezaji wangu viwango vyao vimezidi kuwa juu, ambapo ukiachana na wengine kwa sasa Carlinhos na Yacouba kwa pamoja wameiva sana.

 

“Ni matumaini yangu kama ligi ikirejea watakuja kufanya maajabu kufuatia hali zao za kwendana na program za mazoezi kukubali, kwani kila aliyekaribu nao anaweza kuthibitisha kuwa sasa vijana hawa wameiva na kwamba mimi naendelea kuwaombea kwa Mungu hadi ligi itakaporudi waje kuwa tishio zaidi,” alisema Mwambusi.

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

 

Leave A Reply