The House of Favourite Newspapers

CAS Yasogeza Mbele Hukumu ya Morisson vs Yanga

0

TAREHE ambayo hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Bernard Morrison ilikuwa imepangwa, imesogezwa tena mbele mpaka Novemba 23, mwaka huu.

 

Wakili wa Yanga, Alex Mgongolwa akizungumza, ametoa ufafanuzi kuwa hukumu hiyo itatolewa siku yoyote kuanzia sasa mpaka Novemba 23, kwa mujibu wa taarifa waliyopewa na CAS.

 

Mahakama hiyo ya Usuluhishi wa michezo imetoa maamuzi hayo kutokana na upande wa mawakili wa Bernard Morrison kutuma barua ya kielektroniki (E-mail) huko CAS, ambapo walitoa pendekezo kesi hiyo itolewe hukumu kwa kuwa imekua ikiahirishwa mara kwa mara.

 

Awali CAS ilisema itatoa hukumu ya shauri hilo Oktoba 26, lakini haikutoka na itatoka wakati wowote kutoka sasa mpaka Novemba 23.

 

Leave A Reply