The House of Favourite Newspapers

ads

Casemiro Aipa Pigo Man United baada Kuonyeshwa Kadi Nyekundu

0

MANCHESTER United, inaenda kupata pigo kwa kumkosa staa wake, Casemiro katika mechi nne zijazo baada ya kiungo huyo kuonyeshwa kadi nyekundu.

Casemiro alipata kadi nyekundu katika mchezo wa Premier dhidi ya Southampton uliopigwa juzi Jumapili baada ya kucheza rafu mbaya.

Kadi hiyo Casemiro alipata katika kipindi cha kwanza na kusababisha Man United kucheza pungufu kwa muda mrefu wakati mechi ikiisha 0-0.

Hii imekuwa mara ya pili kwa Casemiro msimu huu kupata kadi nyekundu, awali alipata kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace.

Casemiro sasa atakosekana kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Fulham, kisha atakosekana katika Premier League dhidi ya Newcastle United, Brentford na Everton.

Mara baada ya mchezo dhidi ya Southampton, Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, alisema: “Timu yangu imepambana na wameonyesha kitu licha ya kuwa 10 uwanjani.

“Lakini pia hofu yangu ni Alejandro Garnacho kuhusu hali yake kwa sababu ameondoka uwanjani akiwa anatembelea magongo, tutaendelea kumuangalia zaidi.”

MAPITO ya IMELDA wa GLOBAL TV, KUTIMULIWA na WALINZI wa DIAMOND, UGOMVI na WEMA, MIAKA 21 OFISINI..

Leave A Reply