CASTO ATAMANI NDOA

Casto Dickson

MTANGAZAJI wa CloudsTV, Casto Dickson amefunguka kwamba anatamani kuoa hata leo ila tatizo bado hajajua ni mwanamke gani atakayemuoa kwa sababu kila mwanamke anayekutana naye ana sifa ambazo hazipendi.  

 

Casto ambaye awali alikuwa na uhusiano na Video Queen maarufu Bongo, Tunda Sebastian kisha penzi lao kuvunjika, aliliambia Risasi Mchanganyiko

kuwa, ni kweli ana hamu ya kuoa, lakini tatizo linakuja kwa wanawake anaotaka kuingia nao kwenye ndoa kwani wengi wao hawako tayari na wengine kuna vitu wanavitaka hivyo mwisho wa siku inashindikana.

 

“Unajua mimi siyo mhuni kama ambavyo watu wananifikiria, mimi ni mwanaume ninayejielewa na najua nini nafanya. Ndiyo maana huwa siruhusu hata siku moja kuyumbishwa na maneno ya mtu, kiukweli natamani sana kuoa tena ikiwezekana hata kesho ila tatizo ni kwamba bado sijapata mwanamke sahihi, wengi wao wanapenda starehe tu na siyo vitu vingine vya maana,’’ alisema Casto.

Stori: Memorise Richard

Loading...

Toa comment