Casto: Tunda Ameniharibia Sifa Yangu

MTANGAZAJI maarufu Bongo, Casto Dickson ameweka wazi kuwa hataki mazoea na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Tunda Sebastian kwa sababu alimharibia sifa yake.

 

Akistorisha na Showbiz, Casto alisema hataki mazoea na Tunda kwani amemharibia sifa yake kutokana na kusambaa kwa picha zilizokuwa zikionyesha meseji zilizodaiwa kuwa ni za kwake alizokuwa akimtumia Tunda kisha mwanadada huyo kusema kuwa Casto anamsumbua.

 

“Kiukweli kabisa niseme tu sitaki mazoea na huyo Tunda, kwanza ameniharibia sifa yangu kwa asilimia kubwa na nimtahadharishe tu atakaponiona popote asithubutu hata kunisalimia kwani kitakachotokea hata mwenyewe sijui itakuwaje,” alisema Casto.

AMMAR MASIMBA

 

Toa comment