The House of Favourite Newspapers

Cathy akataa ndoa yake kuwa ‘action and cut’

0

Imelda Mtema

Mambo ya ndoa! Mwigizaji wa kitambo ambaye ni zao la kundi la zamani la Nyota Ensembels lililokuwa likirusha michezo yake kupitia Runinga ya ITV, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa yeye ni msanii lakini maisha ya kisanii hayapeleki kwenye ndoa yake kwani ndoa siyo mambo ya ‘action and cut’ kama wanavyofanya lokesheni.

Mwigizaji wa kitambo, Sabrina Rupia ‘Cathy’.

Cathy ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, ndoa nyingi za mastaa huwa hazidumu kwa sababu huchukua maisha ya nje ya ndoa na kuyapeleka kwenye ndoa ndipo wanapojikuta wakishindwa kudumu ndani ya ndoa kwa muda mrefu.
“Maisha ya ndoa hayahitaji mambo ya kisanii kabisa kwa kuwa wanaume wengi hawapendi mambo hayo,” alisema Cathy.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply