The House of Favourite Newspapers

Cathy Atupa Kule Sanaa

Sabrina Rupia ‘Cathy’.

MKONGWE wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameamua kutupa sanaa kule kisha kujiweka pembeni kwa kile alichosema kwamba, hailipi na amejikita zaidi kwenye kuuza chakula.

 

Cathy aliiambia Za Motomoto News kuwa, kwa sasa amejikita kwenye kupika vyakula ambavyo anasambaza sehemu mbalimbali anapopata oda na imekuwa ikimlipa tofauti na filamu hivyo ameiweka sanaa pembeni kwanza maana kazi ya kupika haina umri na wala haimtupi mtu.

 

“Kupika na kuuza chakula sasa hivi ndiyo habari ya mjini, kwa sasa akili na nguvu zangu zote nimezielekeza kwenye kazi hii ya kupika maana maisha ni magumu sana nikitegemea sanaa tu na nina watoto nitafeli,” alisema Cathy.

STORI: GLADNESS MALLYA | RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.