CBE Yashika Nafasi ya Nane Ubora Vyuo Elimu ya Juu
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, wakati wa kongamano la kitaaluma lililofanyika chuoni hapo.
Alisema chuo hicho kikongwe kimetimiza miaka 60 ya kubobea kwenye kufundisha biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA na kwa muda wote wa uhai wake kimemudu kuzalisha idadi kubwa ya wataalamu wa kada mbalimbali.
Alisema kwa sasa chuo hicho kina kampasi nne za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya na mwakani kinatarajia kujenga kampasi yake nyingine mkoani Kilimanjaro kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni zake.

Alisema katika kudhihirisha ubora wake utafiti uliofanyika mwaka jana ulionyesha chuo hicho kushika nafasi ya nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu nchini na kwamba mafanikio hayo yamewezeshwa kwa mshikamano na walimu na wanafunzi.
Alisema 2018 kampasi zote nne zilikuwa na jumla ya wanafunzi 7,000 lakini kwa sasa wako 23,111 na program 68 katika Nyanja za uchumi, biashar, uongozi TEHAMA na vipimo.

“Tulianzisha program atamizi ili wanafunzi wenye bunifu zao za biashara wazilete tuziatamie ziweze kukua na kuwa biashara kubwa, wewe mgeni rasmi ni shahidi wakati unapita kwenye mabanda yetu umeona vijana waliotengeneza mfumo wa umwagiliaji kidijitali na mfumo wa ukodishaji magari,” alisema
Aidha, alisema tangu kuanza kwa program hiyo wanafunzi 770 wameshaleta bunifu zao na wameweza kuzilea na wako katika hatua mbalimbali na wanafunzi walioleta kwa Dar es Salaam pekee ni 361.

“Elimu mnayoipata hapa msiichukulie poa kabisa ni elimu ambayo inaenda kuwapa maisha huko mtaani, siyo lazima mkimbilie katika ajira mnaweza kutumia ujuzi mliopata kujiajiri na mkafanikiwa,” alisema“Msikae kinyonge, mmepata elimu ambayo inaweza kuwafikisha kwenye safari ya kujikwamua kiuchumi, “ alisema



