The House of Favourite Newspapers

CCM Ilala Wakemea Unyanyasaji kwa Watoto, Mapenzi ya Jinsia Moja Yawa Gumzo

0
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala

JUMUIYA ya Wazazi CCM Mtaa Mafuriko kwa Umoja wao Matawi Mawili (BINTI KAMBA &BUNGONI) Desemba 10/12/2022 Iliungana kwa Pamoja Kuukaribisha Uongozi wa Kata kwenye ziara hiyo.

 

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuleta mahusiano mazuri Kwenye Jumuiya ya Wazazi na kuboresha ushirikiano. Kwenye ziara hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Kutokea Kata Comrade SABRY SHARIFF alielezea namna gani mahusiano huweza kujengwa ili kuongeza Wanachama wapya pia uhai wa Jumuiya hio.

 

Kisha kuwasihi wazazi kuwa makini na watoto wao katika malezi kwani kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia, ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo.

Mapenzi ya jinsia moja miongoni mwa wanafunzi wenyewe limekuwa tatizo kubwa katika jamii

Aidha Katibu Elimu Malezi na Mazingira FIRDAUS SIJA JARIBU aliwaasa na kuwapa wosia namna gani wanaweza Kuongeza ufaulu kwenye kata yao na kudhibiti uchochezi wa mmonyoko wa maadili.

 

Ziara hiyo  Iliambatana na Mh.Diwani Viti Maalumu AISHA ISSA ,Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kata Bi.DEVOTHA BANTULAKI Pamoja na Kamati ya Utekelezaji Kata.

Leave A Reply