The House of Favourite Newspapers

CCM WAMALIZA ZIARA YAO CHINA, WARUDI NA UJUMBE MZITO – VIDEO

Msafara wa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, umerejea nchini ukitokea nchini China walikoenda kwa ajili ya Mafunzo Maalum.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Dkt. Bashiru amesema ziara hiyo imewasaidia kujifunza mengi katika nyanja ya maendeleo kupitia Chama mshirika cha Kikomunist.

 

Amesema miongoni mwa mambo waliyojifunza katika ziara yao ni pamoja na mbinu za uwezekaji ambazo zimeisaidia China kuinuka kiuchumi na kwamba China inatumia rasilimali mbadala katika kuzalisha nishati ikiwemo Mabaki ya vyakula

 

Aidha, Ziara hiyo ya Viongozi wa CCM imetumia siku kumi nchini China ambapo lengo lake ni kujifunza mbinu za kiuchumi na kuimarisha umoja kupitia Chama Mshirika cha Kikomunist.

 

VIDEO: MSIKIE BASHIRU AKIZUNGUMZA HAPA

Comments are closed.