CCM Yapitisha Wanachama 374 Kugombea Nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu
Kikao cha halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika mkoani Dodoma, kimepitisha majina ya wanachama 374 wa CCM wanaogombea nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.
Taarifa hiyo imetolewa kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akitoa taarifa ya kikao hicho cha halmashauri Kuu ya CCM.
Amesema zaidi ya wanachama 2,700 waliojitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ambapo nafasi 15 ni kwa Tanzania Bara na na 15 ni kwa upande wa Zanzibar.
Kila baada ya miaka mitano Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya uchaguzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali.