The House of Favourite Newspapers

CCM Yashutumu Tuhuma Zilizotolewa na MCT

0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Januari Makamba, akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi ndogo makao mkuu Mtaa wa Lumumba jijini Dar.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Makamba.

Wanahabari wakichukua matukio.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) January Makamba, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni CCM, ameshutumu kauli ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari MCT, Kajubi Mukajanga, kuwa Chama Cha Mapinduzi hakijathitisha kushiriki mdahalo uliondaliwa kwa ajili ya wagombea nafasi ya urais.

Kiongozi huyo wa juu kisiasa ndani ya CCM ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM yaliyoko jijini Dar es Salam, kuwa chama chao kilipokea mwaliko wa MCT na kujibu kwa barua Septemba 13 mwaka huu.

Alifafanua kuwa barua hiyo kutoka CCM ilijibiwa kwa kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 na kusainiwa na msaidizi wa katibu mkuu , Stephen Msami, hivyo barua hiyo ikapelekwa kwa ‘dispatch’ ambayo nakala yake hadi sasa wanayo.

Makamba alisema kuwa baada ya hatua hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana alifanya kikao cha pamoja na wawakilishi wa MCT kwenye ofisi ndogo za Lumumba ili kutoa maoni ya CCM kuhusu mdahalo huo.

Ameongeza kuwa CCM inasisitiza kwamba John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea nafasi ya urais alikubali kushiriki mdahalo wa wagombea wote hasa vyama vikuu katika nafasi ya urais.

(Habari Picha: Haruni Sanchawa na Denis Mtima/ GPL)

Leave A Reply