The House of Favourite Newspapers

CEO Simba Atoa Ufafanuzi Sakata la Morrison na Gomez

0

 

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa hakuna ugomvi wowote uliopo kati ya mchezaji wao, Bernard Morrison na kocha wa timu hiyo Didier Gomes.

 

 

Imekuwa ikielezwa kuwa, Gomes raia wa Ufaransa hayupo kwenye maelewano mazuri na nyota huyo raia wa Ghana ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.

 

 

Ndani ya ardhi ya Bongo alianza kukipinga ndani ya Yanga ambao wanadai ni mchezaji wao kwa kuwa dili lake la miaka miwili halikuisha na kesi yao kwa sasa ipo kwenye mahakama ya usuluhishi ya kimataifa, (Cas).

 

 

Hakuwa kwenye kikosi ambacho kilikwea pipa kueleka Sudan ambapo kilicheza jana, Machi 6 na kulazimisha sare ya bila kufungana mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

 

Pia hakuwa kwenye kikosi kilichomenyana na JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni mchezo wa ligi jambo ambalo limepelekea habari hiyo kueleza kwamba hapo ndipo ugomvi wao ulianza.

 

 

Barbara amesema kuwa:”Hakuna ukweli kuhusu ugomvi wa kocha na mchezaji wetu Morrison hizo habari ni za uongo na hilo sisi tunajua kwamba si kweli.

 

 

“Alibaki Tanzania hilo lipo wazi ila ilikuwa ni kwa sababu za benchi la ufundi haina maana kwamba yupo na ugomvi na mwalimu.”

Leave A Reply