The House of Favourite Newspapers

CHADA BOY APATA SHAVU NIGERIA

Joseph Januari ‘Chada Boy’

MKALI wa Ngoma ya Waue, Joseph Januari ‘Chada Boy’ amepata shavu la kuwa Mtanzania wa kwanza kufanya shoo katika tamasha kubwa za muziki la Eko nchini Nigeria. Akizungumza na Risasi Vibes, Chada ambaye wengi huwa wanamfananisha na mkali wa muziki nchini Nigeria, Mr. Flavour alisema kuwa, kilichomfanya kupata shavu hilo ni ngoma yake ya Waue.

“Naamini katika muziki. Muziki wangu ulianza kupenya taratibu Afrika Mashariki na baadaye kuingia nchini Nigeria na Ghana kwa hiyo huenda kuchezwa sana huko kumenifanya nitafutwe kwenye tamasha hilo kubwa litakalofanyika katika mji wa Eko,” alisema Chada. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mapema mwezi Machi, mwaka huu.

 

Comments are closed.