Chadema: Hatuna Imani na Polisi Kuwasaka Waliomshambulia Lissu

Viongozi mbalimbali wa Chadema.

CHAMA cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kimeitaka serikali iwaite wapelelezi kutoka nje ili kuwabaini watu waliopanga njama za kumuua Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye hivi sasa anatibiwa katika hospitali jijini Nairobi baada ya kupata matibabu Hospitali ya Dodoma ambako alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 na watu wasiojulikana hadi leo wiki iliyopita.


Viongozi hao wa Kamati Kuu ya Chadema wamesema mbele ya mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi yao iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwamba hawana imani na jeshi la polisi na serikali katika kuwatafuta na kuwabaini waliokula njama za kumshambulia mbunge huyo.


Loading...

Toa comment