The House of Favourite Newspapers

Chadema: Majibu ya Serikali Kuhusu Hali Hasi ya Uchumi ni Dhaifu

0
majibu ya serikali ni dhaifu
Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Kinondoni, Dar es Salaam.

MBUNGE wa jimbo la Kawe kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee,   amesema Watanzania wanapaswa kupima ukweli kuhusu taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi hapa nchini.]

 

Akijibu taarifa ya msemaji wa serikali leo jijini Dar es Salaam iliyotolewa hivi karibuni, alisema haijajibu hata kidogo hoja za  Mbowe na kuitaka serikali kujibu hoja zinazotokana na taarifa ya Benki Kuu nchini (BOT) zinazoonyesha uchumi kuyumba ikilinganisha na miaka ya nyuma.

 

Mdee amesema uchumi wa karne ya sasa  kamwe hauwezi kuendeshwa kibepari kwa matamko ya viongozi na wateule wao,  hivyo ni lazima bunge lisimamie serikali kuu na halmashauri zipewe mamlaka kamili ya kusimamia maeneo yao bila kuingiliwa na serikali.

Kwa taarifa kamili tembelea Global TV Online.

Na: Denis Mtima/ GPL

Leave A Reply