The House of Favourite Newspapers

Chadema Yapania Kumtoa Mahabusu Lema

lema

Godbless Lema (wa pili kushoto) akirudishwa mahabusu.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejipanga kuhakikisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anatolewa mahabusu. lissu

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema hayo kwa waandishi wa habari  jijini Arusha baada ya yeye mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, na viongozi wengine kumtembelea Lema mahabusu anakoshikiliwa tangu Novemba 2, mwaka jana kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. mbowe-1

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Chadema kimesema kinataka mbunge huyo apate haki ya kisheria na kuwa huru kutokana na kukaa mahabusu kwa kipindi hicho kirefu ambapo kitawatumia wananasheria katika kesi mbalimbali zinazomkabili.

Dhamana ya Lema imekuwa ikikwama kutokana na hoja za kisheria zilizosababisha upande wa utetezi uende hadi Mahakama Kuu katika kuhakikisha anapata haki hiyo ambapo hadi sasa bado vita hiyo ya kisheria haijaisha.

Lissu alisema watakiandikia barua rasmi Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kukitaka kitoe tamko kuhusu mgogoro huo na ikiwezekana kitoe mawakili waliopo Arusha kusaidia kesi zinazomkabili Lema.

 “Hawa wanasheria wasijidai hamnazo wakati mbunge wao yupo mahabusu. Tutawaambia wawepo mahakamani, kwa kuwa wananchi  wa kawaida hawaruhusiwi kuja kusikiliza kesi hiyo, basi wanasheria hao waje,” alisema Lissu.

 

Salum milongo/GPL

 

 

Comments are closed.