The House of Favourite Newspapers

Chalenji yavuruga kikosi Yanga

0

YANGA-MTIBWA-11.jpg

Wilbert Molandi,

Dar es Salaam

IMEELEZWA kuwa michuano ya Kombe la Chalenji imezuia kambi na mechi za kirafiki za kimataifa kwa Yanga ilizopanga icheze kama matayarisho ya Ligi Kuu Bara.

Michuano hiyo ya Chalenji imepangwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21, mwaka huu huko nchini Ethiopia.

Yanga hivi sasa inaendelea na maandalizi ya ligi kuu chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van Der Pluijm na Juma Mwambusi wakati ligi hiyo ikisimama.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema ni ngumu kuifuata programu aliyoipanga wakati ligi kuu ikisimama kutokana na nusu ya wachezaji kuwepo vikosi vya timu zao za taifa.

Pluijm alisema, katika ripoti yake aliomba mechi tano za kirafiki za kimataifa pamoja na kambi ya pamoja ya kujiandaa na ligi hiyo katika kuhakikisha wanautetea ubingwa wao.

“Timu inaendelea na mazoezi yake ya pamoja ikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wa U-20 baada ya nusu ya wachezaji wa timu kubwa kuwepo kwenye timu zao za taifa.

“Hivyo hivi sasa siwezi nikafanya chochote ikiwemo kucheza mechi za kirafiki za kimataifa, pamoja na kambi ya kujiandaa na ligi kuu iliyosimama hadi pale wachezaji wote watakaporejea kujiunga na wenzao,” alisema Pluijm.

Leave A Reply