Kartra

Chama Aandaliwa Program Maalum Simba

 

KUFUATIA changamoto ya msiba wa mke wake, kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameandaliwa programu maalum na uongozi wa benchi la ufundi la klabu hiyo itakayomsaidia kurejea katika makali yake pale atakapojiunga na kikosi.

 

Taarifa za Chama kufiwa na mke wake zilithibitishwa na uongozi wa Simba Mei 29, mwaka huu ambapo taratibu zote za mazishi zilifanyika kwao nchini Zambia.

 

Akiwa na kikosi cha Simba msimu huu Chama amekuwa katika kiwango bora, ambapo katika michuano ya Ligi Kuu Bara pekee msimu huu, amehusika kwenye mabao 20 ya Simba, akifunga mabao saba na kuasisti mara 13.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha wa Viungo wa Simba, Adel Zrane, alisema: “Unajua utimamu wa saikolojia ni muhimu sana kwa mchezaji ili aweze kufanya vizuri, mchezaji anaweza kuandaliwa katika kila eneo lakini kama saikolojia yake haitakuwa sawa basi hawezi kufanya vizuri.

 

“Kama kikosi tumesikitishwa sana na tukio la Chama kumpoteza mke wake, ni jambo gumu na tayari kama benchi la ufundi tumeandaa programu maalum ya kumjenga kiakili na kimwili ili kumsaidia arejee katika kiwango chake pale atakapojiunga na kikosi.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam


Toa comment