Chama Abariki Luis Kujiunga na Al Ahly

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama, amefunguka kuwa atamsapoti mchezaji mwenzake na rafiki yake mkubwa, Luis Miquissone ikiwa nyota huyo atafanya maamuzi ya kukubaliana na ofa
ya kujiunga na
Mabingwa wa Afrika, Al Ahly.


Al Ahly
wamekuwa wakiiwinda saini ya Luis kwa muda mrefu sasa kufuatia mapendekezo ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Pitso Mosimane, na hivi karibuni imeripotiwa kuwa wapo tayari kuwasilisha ofa ya dola 900,000 sawa na shilingi bilioni 2 za Kitanzania ili kufanikisha dili hilo.

 

Mosimane amewahi kumfundisha Luis katika Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kabla ya Luis kujiunga na Simba huku Mosimane akitimkia Misri.

 

Luis msimu huu amekuwa katika kiwango kikubwa akifanikiwa kuhusika kwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara pekee, ambapo alifunga mabao tisa na kuasisti mabao 10.Akizungumza kuhusiana na dili hilo, Chama alisema:

 

“Kuhusiana na suala la Luis kujiunga na Al Ahly, nadhani hilo ni juu yake kuchagua kama ataondoka, au atasalia Simba, ni kweli Luis ni rafiki yangu, hivyo nitamshauri aangalie sehemu anayoona kwake inamfaa.

 

“Kama akiamua kuondoka nitamuunga mkono, na kama akitaka kubaki nitamuunga mkono pia, hivyo tumuachie yeye na uongozi ufanye maamuzi.”702
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment