Chama Afunika Yanga Kwa Asisti Ligi Kuu

MSIMU wa Ligi Kuu Bara 2020/21 ndiyo hivyo umeshatupungia mkono wa kwaheri ambapo hapo jana ilipigwa michezo ya mzunguko wa 34, na wa mwisho kabisa.

Kilichofuata baada ya hapo ni utofauti wa shangwe lililoshushwa na bingwa mtetezi klabu ya Simba pamoja na wale walioponea kwenye tundu la sindano kushuka daraja na vilio ambavyo wpasi nyingi za mwisho asisti kwenye Ligi Kuu Bara kama ifuatavyo;

 

CHAMA ASISTI 15

Kiungo mshambuliaji wa Simba na mtetezi wa tuzo ya mchezaji bora aliyoitwaa mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kuhusika kwenye mabao 15.Msimu huu nyota huyo raia wa Zambia ameonekana kuwa na moto zaidi ambapo kabla ya mchezo wa jana Jumapili alikuwa amehusika kwenye mabao 23, akifunga mabao nane na kuasisti mara 15, hivyo bila shaka anajiweka katika nafasi nzuri ya kutetea tuzo nne alizotwaa msimu uliopita.

LUIS MIQUISSONE 10

Nyota wa kimataifa wa Simba ambaye ni raia wa Msumbiji, Luis Miquissone naye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu kiasi cha kushawishi klabu mbalimbali kubwa Afrika kufikiria namna ya kuipata saini yake.Luis msimu huu kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara pekee amefanikiwa kuasisti mara 10 hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa nyota waliiohusika kwenye mabao mengi ambapo kabla ya mchezo wa jana alikuwa amehusika katika mabao 19, akifunga mabao tisa.

 

IDDI SELEMANI NADO 8

Ukizungumzia nyota wa Azam waliofanya vizuri zaidi msimu huu, basi ni wazi huwezi kuacha kulitaja jina la kiungo mshambuliaji Nado ambaye msimu huu amefanikiwa kuifungia Azam mabao 10.

Nyota huyo hakuishia kwenye kufunga pekee bali pia akiwa amehusika kwenye mabao mengine nane kwa kutoa asisti.Bila shaka hii ndiyo sababu kubwa ya uongozi wa Azam kuamua kumuongezea mkataba wa miaka miwili nyota huyo ambao utamfanya aendelee kusalia mpaka mwaka 2014.

 

RAJABU ATHUMAN 8

Kiungo kinda wa klabu ya Gwambina ambaye naye amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu akiwa anakamatia nafasi ya nne katika orodha ya nyota waliotoa asisti nyingi msimu huu baada ya kufanya hivyo mara nane sawa na Nado wa Azam.Akiwa na umri wa miaka 20 tu kwa sasa, bila shaka kama atapata mazingira mazuri ya kujiendeleza kipaji chake kuna mambo mengi ya kutarajia kutoka kwake.

 

ABDULRAHMAN MUSSA 7

Kutoka ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting mshambuliaji wao Abdulrahman Mussa si tu ametimiza majukumu yake ya kushambulia kwa kufunga mabao, lakini pia ameonyesha uwezo wa kuasisti mabao kwa wenzake ambapo aliweza kutoa asisti saba kabla ya mchezo wa jana.

DAVID LUHENDE 6

Anatajwa kuwa mlangoni kuibukia ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara klabu ya Simba, hii ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa akiwa na Kagera Sugar msimu huu ambapo nyota huyo amefanikiwa kuasisti mara saba, akiwa ndiye mlinzi pekee kwenye orodha hii ambaye amefanikiwa kufanya hivyo.

DICKSON AMBUNDO 7

Winga wa klabu ya Dodoma Jiji ambaye inaelezwa kuwa tayari amemalizana na uongozi wa klabu ya Yanga kwa ajili ya kutoa huduma yake kwa Wananchi msimu ujao. Kama dili hilo litafanikiwa basi ni wazi uhamisho huo hauwezi kuwa kwa bahati nasibu bali ni kutokana na takwimu nzuri za Ambundo msimu huu ambapo amehusika kwenye zaidi ya mabao kumi, ikiwemo asisti saba alizotoa.

 

DEUS KASEKE 6

Huyu ni miongoni mwa wachezaji waandamizi ndani ya klabu ya Yanga ambayo amehudumu kwa mafanikio makubwa kwa muda mrefu. Msimu huu Kaseke amehusika kwenye mabao 12 ya Yanga ambapo amefunga mara sita na kuasisti mara sita.Kasi yake hiyo imeufanya uongozi wa Yanga kufikia maamuzi ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili kuhudumu ndani ya kikosi hicho.

 

RALLY BWALYA 6

Kiungo mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba aliyejiunga nao akitokea Power Dynamo ya Zambia, naye hayupo nyuma ambapo licha ya kwamba huu ni msimu wake wa kwanza lakini amefanikiwa kutoa asisti sita kwenye mkichuano ya Ligi Kuu Bara pekee.

TUISILA KISINDA 5

Mkata upepo wa Yanga ambaye huku mtaani wamembatiza jina la kipimo cha umri kutokana na mwendokasi wake unaoonekana kuwashinda walinzi wengi anaokutana nao.Tuisila msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara pekee ametoa asisti tano.


Toa comment