Chama Amtaja Fei Toto, Ajibu Yanga

KIUNGO mwenye vionjo vya kipekee ndani ya kikosi cha Simba, Claytous Chama raia wa Zambia ameweka wazi kwamba ndani ya kikosi cha Yanga kuna wachezaji watatu anaowazimia akiwemo Ibrahim Ajibu.

 

Chama ambaye amekuwa na msaada mkubwa ndani ya Simba, amekuwa akifananishwa

na Ajibu kutokana na aina yao ya uchezaji uwanjani huku wote wakiwa na vikorombwezo vingi.

Kiungo huyo wa zamani wa Power Dynamos ya Zambia, ametamka wazi kuwa ndani ya Yanga anawakubali Ajibu, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Kelvin Yondani.

 

Chama mwenye miaka 27, amesema kwamba anakoshwa na Ajibu ndani ya kikosi hicho cha Yanga kinachonolewa na Mkongo, Mwinyi Zahera.

 

Kiungo huyo ambaye kwa sasa ana mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, amefafanua kwa kusema: “Wachezaji ambao ninawazimikia pale Yanga ni Ibrahim Ajibu, Fei Toto sambamba na Yondani.”

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment