The House of Favourite Newspapers

Chama Amuibua Fei Toto Yanga

0

KIUNGO wa Yanga Feisal Salum amesema kuwa anaamini msimu ujao utakuwa msimu bora kwa mashabiki wa Yanga kushuhudia akiondoka na tuzo nyingi ikiwemo ile ya kiungo bora iliyochukuliwa na kiungo wa zamani wa Simba, Clatous Chama.

Katika tuzo za TFF ambazo zimetolewa hivi karibuni Feisal Salum, alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam huku akifanikiwa pia kuingia katika kikosi bora cha ligi kuu cha msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Feisal alisema kuwa anatamani kuona msimu ujoa akishinda tuzo za kiungo bora wa msimu ambayo imechukuliwa na Chama na mchezaji bora wa msimu huku akiwaahidi mashabiki wa Yanga msimu ujao watarajie kupokea tuzo nyingi kutoka kwake.

“Nashukuru Mungu kwa hiki ambacho nimekipata kwa msimu uliopita wa ligi kuu, nimefurahi sana na malengo yangu kwa sasa ni kuhakikisha nafikia ndoto zangu za kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu na ile ya kiungo bora wa msimu.

“Najua haitakuwa kazi nyepesi lakini naamini kila kitu kitawezekana pale ambapo kutakuwa na juhudi, mashabiki wa Yanga waendelee kutusapoti kwani msimu ujao watapata tuzo nyingi kutoka kwangu,” alisema kiungo huyo.

Leave A Reply