The House of Favourite Newspapers

Chama Aweka Rekodi CAF, Abeba Tuzo Mbele Ya Mastaa Wa Raja

0

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Mzambia, Clatous Chama, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Wiki ya Raundi ya Nne ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mzambia huyo amechaguliwa kuwa mchezaji bora, wakati timu hiyo, ilipovaana dhidi ya Vipers SC wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Chama alifunga bao la ushindi uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofutia ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa Mtandao wa CAF, Chama ameshinda tuzo hiyo akiwashinda Peter Shalulile anayeichezea Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.

Mwingine ni Ahmed Zizo anayeichezea Zamalek ya nchini Misri na Walid Sabbar wa Raja Casablanca ya Morocco.

Wakati kiungo huyo akishinda tuzo hiyo, pia juzi aliweka rekodi ya kwanza ya kuingia katika kikosi bora cha Raundi ya Nne akiwa pamoja na beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe.

Chama keshokutwa Jumamosi anatarajiwa kuingoza timu yake, katika mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi C watakapovaana dhidi ya Horoya AC kwenye Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kupata ushindi ili ijiweke katika nafasi ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leave A Reply