The House of Favourite Newspapers

Chama, Aziz KI Kivumbi Kwenye Msako wa Kiungo Bora Ligi Kuu Bara

0
Clatous Chama

STEPHANE Aziz Ki, kiungo wa Yanga na Clatous Chama wa Simba, ni miongoni mwa viungo watakaotimua kivumbi kwenye msako wa kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Aziz KI ametwaa taji la ligi akiwa na uzi wa Yanga baada ya timu hiyo kufikisha pointi 74, ikiwa na mechi mbili mkononi, huku Chama na Simba yake wakigotea nafasi ya pili.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wachezaji hao wapo kwenye kipengele cha kiungo bora.

Chama ana mabao manne na pasi 14 za mabao akiwa ni kinara wa kutengeneza pasi za mwisho, huku Aziz KI akiwa ametupia mabao 9 na pasi tano za mabao.

Aziz KI

Wengine ni Mzamiru Yassin wa Simba ambaye amefunga mabao mawili na kutoa pasi tano za mabao , Bruno Gomes wa Singida Big Stars katupia mabao 9 na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ wa Simba katupia mabao 10, ana pasi 12 za mabao.

Mbali na kivumbi hicho, pia kwenye anga la msako wa beki bora, Henock Inonga, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe  wote wa Simba, amepenya kwenye orodha hiyo, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto hawa wa Yanga.

Kwa upande wa Tuzo ya MVP, Mzamiru Yassin na Saidi Ntiazonkiza ‘Saido’ wa Simba, Fiston Mayele na Djigui Diarra wa Yanga, Bruno Gomes wa Singida Big Stars.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

FAHAMU KITUO HIKI CHA WATOTO YATIMA WAMILIKI BIBI na BABU -CHARMING CHARITY WAWAFIKIA KUTOA MSAADA..

Leave A Reply