The House of Favourite Newspapers

Chama, Baleke Wapewa Sh 250Mil Wawamalize Horoya, Kikao Kizito Chafanyika

0
Kikosi cha timu ya Simba.

WACHEZAJI wa Simba wakiongozwa na mastaa Jean Baleke na Clatous Chama wanahitaji ushindi wa aina yoyote leo ili wapate bonasi ya Sh 250Mil walizowekewa na mabosi wa timu hiyo.

Simba leo wanatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana dhidi ya Horoya AC katika mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo, Simba wanahitaji ushindi wowote ili wajiweke katika nafasi ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jean Baleke

Mmoja wa mabosi wa Simba, kutoka ndani ya Benchi la ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumamosi kuwa mabosi na wachezaji hao walitarajiwa kukutana jana Ijumaa kufanya kikao sambamba na kula chakula cha jioni kambini kwao Mbweni nje kidogo ya Dar.

Bosi huyo alisema kuwa, kikao hicho kitakuwa cha kuwapa hamasa na morali kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha wanapata ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri.

Clatous Chama

Aliongeza kuwa wachezaji kwa pamoja chini ya Nahodha Mkuu wa timu hiyo, John Bocco wameahidi kupambana ili kufanikiwa malengo yao ya kufuzu robo fainali.

“Bodi ya Wakurugenzi kwa pamoja leo (jana) usiku wanatarajiwa kukutana na wachezaji, benchi la ufundi mara baada ya mazoezi ya jioni kwa ajili ya kufanya kikao kifupi kambini.

“Kikao hicho maalum kwa ajili ya kuwapa hamasa pamoja na kuwapa bonasi ya Sh 250Mil watakazopewa kama wakifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Horoya.

“Fedha hizo ni tofauti na zile ambazo walizoahidiwa na na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan za kila bao Sh 5Mil atakazowapa baada ya kufunga bao,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Bonasi ipo kwa wachezaji katika kila mchezo ambayo inatofautiana na ukubwa wa mechi.

“Kuelekea mchezo wetu dhidi ya Horoya ni lazima iwepo utofauti ya bonasi kwa wachezaji wetu, na hiyo ni kutokana na umuhimu wa mchezo huo,” alisema Ally.

STORI: WILBERT MOLANDI

RAIS SAMIA AWATAKA WASANII KUHAMASISHA KILIMO, AMTAJA ALIKIBA na MRISHO MPOTO…

Leave A Reply