Chama cha Labour chashinda uchaguzi mkuu wa Uingereza
Chama cha Labour kimeshinda rasmi uchaguzi mkuu wa Uingereza 2024 baada ya kufikisha viti 326 vinavyohitajika.
Waziri Mkuu mteule wa Uingereza Keir Starmer ameahidi kuanza “enzi mpya ya kitaifa” baada ya Chama chake cha Labour kumaliza utawala wa Conservative uliodumu kwa miaka 14.
Baada ya uchaguzi wa jana Julai 4, 2024, Starmer kutoka Chama cha Labor aliibuka kidedea na kumbwaga aliyekuwa Waziri Mkuu Rishi Sunak wa Conservative.
Vyama vingine vilivyohusika kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Reform UK, Liberal Democrats, Democratic Unionist Party, Green, Scottish National Party (SNP) na Plaid Cymru na vinginevyo.
Starmer anakabiliwa na changamoto ya kushughulikia masuala mbalimbali yakiwemo ukuaji wa uchumi, afya, uhalifu, ulinzi na usalama, makazi na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (Brexit).