The House of Favourite Newspapers

Chama Hatari Yake Dakika 123, Ahusika Kwenye Mabao 13

0

 

MWAMBA wa Lusaka Clatous Chama ndani ya msimu wa 2023/24 hatari yake ilikuwa kila baada ya dakika 123 ndani ya uwanja kutokana na kuhusika kwenye mabao 13.

Ipo wazi kuwa ulikuwa ni msimu mbavu kwa Simba kwenye rekodi kutokana na kuwa ni timu ambayo imefungwa mabao mengi ndani ya nne bora ambayo ni 25 baada ya mechi 30.

Ukiweka kando kuruhusu mabao mengi iliporomoka kutoka nafasi ya pili iliyogotea msimu wa 2022/23 ikigotea nafasi ya tatu na pointi zake 69 sawa na Azam FC wakitofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Chama ni dakika 1,610 alipata kucheza kwenye mechi 21 kati ya 30 ambazo Simba ilicheza akikosekana kwenye mechi 9 pekee kwa msimu wa 2023/24.

Ni mabao 7 nyota huyo alifunga akitoa pasi sita za mabao kinara wa utupiaji ndani ya Simba ni Saido Ntibanzokiza ambaye alifunga mabao 11.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

MZEE MWENDA AWAKA na VIONGOZI wa SIMBA – “KWA NINI WANANG’ANG’ANIA TIMU YETU?”….

Leave A Reply