Chama, Kagere Mtegoni Simba
MASTAA wa Simba wamewekewa mtego mzito na kocha wao Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ambao utalipuka mara baada ya timu hiyo itakapoanza mazoezi yao ya pamoja.
Mbelgiji huyo ametoa program kwa kila mchezaji kwa ajili ya kujiweka fiti katika kipindi hiki ambacho Virusi vya Corona vimepambana moto huku Ligi Kuu Bara na nyingine zikiwa zimesimamishwa kupisha maambukizi hayo.
Baadhi ya mastaa mbalimbali wameonekana wakitupia mitandano baadhi ya vipande vya video zao zikiwaonyesha wakifanya mazoezi na kati ya hao ni Jonas Mkude, Francis Kahata, Clatous Chama, Meddie Kagere, Pascal Wawa na Aishi Manula.
Akizungum-za na Champi-oni Jumamosi,Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa ni ngumu kwao kujua na kua-mini wachezaji wao wa-nafua-ta program za mazoezi ambazo wamepwa na kocha wao Sven.
Rweyemamu alisema kuwa wamepanga kuwafanyia ‘test’ wachezaji wote kwa lengo la kujiridhisha ni kweli walikuwa wanafanya program hizo za mazoezi katika kipindi hiki ligi ikiwa imesimama.
“Ni ngumu kwa sasa kuamini kuwa wachezaji wanafuata program za kocha vile inavyowataka kufanya, hivyo tumepanga siku tukikutana tutafanya testi ili kujua kama wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi, na walikuwa wanafanya kwa kiwango kile ambacho kocha alitaka.
“Tunafuatilia kwenye mitandao mazoezi yao kwa sababu wanatutumia, lakini sisi tumejiwekea masharti kuwa mazoezi rasmi yataka-poanza itabidi tujiridhishe.“Lakini tunaamini kabisa wachezaji wanafuata vema program hizo za mazoezi walizopewa, kwani soka ndiyo ajira yao,” alisema Rweyemamu.



