The House of Favourite Newspapers

Chama la Simba Hili Hapa

0

TAYARI kwa sasa mashabiki wa Simba wapo na shauku kubwa kuona namna gani watajitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa, Dar, kushuhudia chama lao likitambulishwa pamoja na burudani za kutosha.

Itakuwa leo Septemba 19, 2021 ambapo Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, aliliambia Spoti Xtra kuwa, kila kitu kipo katika mpangilio ulivyo, ni suala la mashabiki kununua tiketi kwa wingi na kujitokeza kushuhudia burudani siku hiyo.

Katika Tamasha la Simba, timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Hapa Spoti Xtra linakuletea chama kamili la Simba kwa msimu wa 2021/22 pamoja na wale warithi wa mikoba ya nyota ambao walisepa.

 

MAKIPA

Aishi Manula na Beno Kakolanya hawa kwa upande wa makipa waliweka rekodi ya kuwa timu iliyoruhusu mabao machache ya kufungwa ambayo ni 14 katika mechi 34 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Manula ni kipa bora wa Simba ambapo hata msimu uliopita wa 2019/20, alikusanya clean sheet 18.

Msimu wa 2020/21 alikusanya clean sheet 18 akicheza mechi 26 kati ya 34, alitumia dakika 2,278, huku Kakolanya akikaa langoni mechi 8. Kazi kubwa ni kuendeleza rekodi yao msimu ujao na Ally Salim alikwama kuanza langoni.

 

MABEKI

Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Joash Onyango, hawa wana kazi ya kuendelea pale ambapo waliishia. Kinara wa pasi za mwisho alikuwa ni Kapombe ambaye alitoa pasi sita na alicheza mechi nyingi sawa na Tshabalala ambao kila mmoja alicheza mechi 31.

Ukuta bora kwa msimu uliopita ulikuwa ndani ya Simba kwa kuwa waliruhusu mabao 14 katika mechi 34.

 

VIUNGO

Jonas Mkude, Rally Bwalya, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu na Taddeo Lwanga, hapa kesi kubwa iliyokuwa inatibulia viungo ni ile ya utovu wa nidhamu hasa kwa Mkude ambaye aliweza kusimamishwa mara mbili.

 

WASHAMBULIAJI

Utatu ambao ulikuwa kwenye moto na kutupia jumla ya mabao 44 msimu uliopita, ni Meddie Kagere aliyefunga mabao 13, Chris Mugalu (15) na kinara wao, Jonh Bocco (16). Jumla timu hiyo ilifunga mabao 78.

 

WABEBA MIKOBA

Katika maingizo mapya ya Simba, kuna wawili ambao wanatajwa kupewa mikoba ya nyota waliosepa ndani ya timu hiyo wakiwa wameacha alama kubwa msimu uliopita.

Ni Clatous Chama na Luis Miquissone ambao walikuwa mhimili wa timu hiyo kwa upande wa viungo kutokana na kazi ambayo waliifanya.

 

Kiungo Peter Banda anatajwa kuwa mrithi wa Luis. Ana kazi ya kufanya makubwa ila haitakuwa kazi rahisi kwake kwa kuwa itahitaji muda kufikia ubora unaotakiwa.

 

Ikumbukwe kwamba Luis kwa msimu uliopita katika ligi kuu alikuwa namba mbili kwa wapiga pasi za mwisho ambapo alikuwa nazo 10 na kufunga mabao 9.

 

Sakho anatajwa kuwa mrithi wa Chama, naye pia ana kazi ya kufanya kwa ajili ya kutimiza majukumu yake. Ikumbukwe kuwa Chama alikuwa ni kiungo bora wa muda wote ndani ya Simba. Msimu wa 2019/20 alikuwa ni kiungo bora alipofunga mabao mawili na pasi za mwisho 10.

 

Msimu wa 2020/21 Chama alifunga mabao 8 na pasi za mwisho 13, hivyo sio kazi nyepesi kwa mrithi wa Chama kufanya kazi kama ya mwamba huyo wa Lusaka.

 

WANAOSUBIRIWA KUTAMBULISHWA

Jeremiah Kisubi, huyu ni kipa, inaelezwa kuwa ameshamalizana na Simba, ni suala la muda tu kutambulishwa akitokea Prisons, sawa na mshambuliaji, Kibu Denis kutokea Mbeya City.

 

HAWA HAPA UHAKIKA

Waliotambulishwa rasmi ni Peter Banda, ametokea Big Bullet ya Malawi na Yusuph Mhilu aliyekuwa Kagera Sugar.

Wengine ni Duncan Nyoni aliyekuwa Silver Strike ya Malawi, Pape Ousmane Sakho (Tenghueth), Henock Inoga Baka (DC Motema Pembe), Israel Mwenda (KMC), Abdulswamad Kassim (Kagera Sugar), Emmanuel Mwanuke (Gwambina) na Sadio Kanoute (Al-Ahli Benghazi).

LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply