The House of Favourite Newspapers

Chama, Luis Waitikisa Yanga

0

IKIWA wikiendi hii watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana Uwanja wa Mkapa, Dar, rekodi zinaonesha kuwa nyota wawili wa Simba, Clatous Chama na Luis Miquissone wanaitikisa Yanga kwa takwimu zao za kufunga na kutoa pasi za mabao.

 

Wawili hao Simba ikiwa imefunga mabao 58, Clatous Chama amefunga mabao 7 na kutoa asisti 13, huku Luis akifunga mabao 7 na asisti 9.

 

Chama amehusika kwenye mabao 20 na Luis mabao 16 na kuwafanya wote wahusike kwenye mabao 36 rekodi ambayo haijafikiwa na nyota wa Yanga.Yanga, kinara wao ni Yacouba Songne aliyefunga mabao sita na ametoa asisti nne, akifuatiwa na Mukoko Tonombe mwenye mabao manne na asisti nne katika mabao 41 ya Yanga.

Licha ya takwimu za Simba kuwa katika hali ya kutisha, beki wa zamani wa kikosi hicho na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Boniphace Pawasa, amelimbia Spoti Xtra kuwa mchezo wa Simba na Yanga huwa na matokeo ya kushangaza.

 

“Ikiwa utasema utazame ubora huwa haiwi hivyo, kwenye mechi za Simba na Yanga, wachezaji wasipoangalia wanaweza kufanya vizuri ama kutolewa kwenye ramani.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA,

Leave A Reply