Chama: Niliwatamani Sana RS Berkane

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Mzambia, Clatous Chama ameweka wazi kuwa alitamani sana kuwa sehemu ya timu yake ambayo itavaana na RS Berkane kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika leo Jumapili.

 

Simba ambao ni vinara wa msimamo wa kundi D la michuano hiyo, leo Jumapili saa 4:00 usiku watashuka kwenye Uwanja wa Manispaa ya jiji la Berkane kukipiga dhidi ya Berkane ya Morocco.

 

Chama ambaye alirejea Simba kwenye dirisha dogo alikuwa anaichezea Berkane ambapo hatocheza mchezo huo kutokana na kubanwa na kanuni la Soka Afrika (Caf).

 

 

Chama alisema: “Tumekuwa na maandalizi mazuri ya mchezo wetu wa leo dhidi ya Berkane, ambapo naona wachezaji wenzangu wana ari kubwa ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

 

“Binafsi nilitamani sana kuwa sehemu ya kikosi ambacho kingecheza mchezo huu na kutoa mchango wangu katika kuisaidia timu, lakini kama ambavyo inafahamika kuwa kanuni haziniruhusu kuwa sehemu ya mchezo huo kama mchezaji.

 

“Lakini nitaendelea kujitoa kwa wachezaji wenzangu na benchi la ufundi kwa taarifa yoyote watakayoihitaji ili kufanikisha malengo yetu ya kushinda mchezo huu.”

4234
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment