Chama: Tutawashangaza JS Saoura

KIUNGO mnyumbulifu wa Simba, Mzambia Claytous Chama ametamba kwamba licha ya ugumu wa kucheza ugenini kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini safari hii watapambana kuondoka na pointi tatu kwa ajili ya kubadili rekodi ya kupoteza mara mbili walipocheza na Al Ahly ya Misri na AS Vita Club ya DR Congo.

 

Mzambia huyo kesho Jumamosi ataiongoza safu ya kiungo ya Simba kupambana na JS Saoura katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba watakuwa ugenini katika Uwanja wa 20 Août 1955 Béchar nchini Algeria.

 

Katika mechi zake mbili zilizopita za ugenini, Simba inayonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems, haikuwa na matokeo mazuri baada ya kupokea vichapo vya mabao 5-0, mbele ya Al Ahly na AS Vita Club.

 

Kiungo huyo amesema wanajua umuhimu wa mechi hiyo mbele ya Saoura ambayo kama wakipata ushindi watajiwekea mazingira mazuri ya kutinga robo fainali ya mashindano hayo makubwa Afrika kwa ngazi ya klabu, hivyo watapambana kwa hali ya juu kushinda na kuweka rekodi mpya wakiwa ugenini.

 

“Kila mmoja miongoni m w e t u anafahamu umuhimu wa mechi hii, tunataka kuweka rekodi mpya ya kushinda ugenini lakini pia kujisogeza kwenye hatua ya kucheza robo fainali. Safari hii tutapambana kwa kiwango kikubwa ili tupate matokeo mazuri,” alisema Mzambia huyo.
Aliongeza

Toa comment