The House of Favourite Newspapers

Chama: Uzoefu Unatubeba Dhidi ya Wydad Casablanca Morocco

0

KUELEKEA mchezo wao wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, kiungo Mzambia wa Simba, Clatous Chama amechimba mkwara mzito kuwa kikosi chao kitafuzu nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na faida kubwa ya uzoefu walionao.

Kesho Ijumaa, Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Mohamed V jijini Casablanca nchini Morocco kurudiana na wenyeji wao Wydad Casablanca kuwania kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba Jumamosi iliyopita wakicheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali ya kwanza.

Akizungumza na Spoti Xtra, Chama alisema: “Malengo yetu ni kufika nusu fainali, tunawaheshimu Wydad ni miongoni mwa timu bora na ngumu, lakini tumejipanga kupambana kupata matokeo mazuri.

“Faida kubwa kwetu ni uzoefu ambao tunao kwenye mashindano haya na hasa ukizingatia siku chache zilizopita tulikuwa Morocco kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya mashindano haya.”

MAPOKEZI ya RAIS wa RWANDA PAUL KAGAME, APIGIWA GWARIDE LA HESHIMA…

Leave A Reply